Faida ya kujua masuala ya imani kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah

Kujua ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah inapokuja katika imani kunamzuia mtu kutumbukia katika upotevu wa kukufurisha kwa kufanya maasi au kwa kukufurisha kwa yasiyokuwa yenye kukafirisha. Kwa hivyo yule ambaye anaelewa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika imani utatengemaa ulimi na akili yake kutokamana na kuingia katika upetukaji mipaka na ukafirishaji na kufuata mapote potofu ambayo yameenda kuwakufurisha waislamu na wakaingiza katika Uislamu na imani wasiokuwa waislamu wala waumini.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 114
  • Imechapishwa: 28/08/2020