182 – Muhammad bin Yahyaa bin Ayyuub bin Ibraahiym ametukhabarisha: ´Abdul-Wahhaab ath-Thaqafiy ametukhabarisha: Khaalid al-Hadhdhaa’ ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Qilaabah, kutoka kwa Anas, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtu mwenye rehema zaidi wao katika ummah wangu kwa ummah wangu ni Abu Bakr. Mshupavu zaidi wao katika amri ya Allaah ni ´Umar. Mwenye aibu zaidi wao ni ´Uthmaan. Mwenye kukisoma zaidi wao Kitabu cha Allaah ni Ubayy bin Ka’b. Mjuzi zaidi wao katika fani ya mirathi ni Zayd bin Thaabit. Mjuzi zaidi wao juu ya halali na haramu ni Mu’aadh bin Jabal. Zindukeni! Hakika kila ummah una mtu mwaminifu. Hakika mwaminifu wa ummah huu ni Abu ´Ubaydah.”[1]
183 – al-Haytham bin Ayyuub ametukhabarisha: Ibraahiym ametukhabarisha: Ibn Shihaab ametukhabarisha, kutoka kwa ´Ubaydah bin as-Sabbaaq, kutoka kwa Zayd bin Thaabit, ambaye amesema:
“Abu Bakr alinitumia ujumbe na kusema: “Wewe ni kijana mwenye hekima. Hatukutuhumu. Ulikuwa ukimwandikia wahy Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo hakikisha unaipatiliza Qur-aan na kuikusanya.”[2]
[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (868).
[2] al-Bukhaariy (4986).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 120
- Imechapishwa: 22/09/2026
182 – Muhammad bin Yahyaa bin Ayyuub bin Ibraahiym ametukhabarisha: ´Abdul-Wahhaab ath-Thaqafiy ametukhabarisha: Khaalid al-Hadhdhaa’ ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Qilaabah, kutoka kwa Anas, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtu mwenye rehema zaidi wao katika ummah wangu kwa ummah wangu ni Abu Bakr. Mshupavu zaidi wao katika amri ya Allaah ni ´Umar. Mwenye aibu zaidi wao ni ´Uthmaan. Mwenye kukisoma zaidi wao Kitabu cha Allaah ni Ubayy bin Ka’b. Mjuzi zaidi wao katika fani ya mirathi ni Zayd bin Thaabit. Mjuzi zaidi wao juu ya halali na haramu ni Mu’aadh bin Jabal. Zindukeni! Hakika kila ummah una mtu mwaminifu. Hakika mwaminifu wa ummah huu ni Abu ´Ubaydah.”[1]
183 – al-Haytham bin Ayyuub ametukhabarisha: Ibraahiym ametukhabarisha: Ibn Shihaab ametukhabarisha, kutoka kwa ´Ubaydah bin as-Sabbaaq, kutoka kwa Zayd bin Thaabit, ambaye amesema:
“Abu Bakr alinitumia ujumbe na kusema: “Wewe ni kijana mwenye hekima. Hatukutuhumu. Ulikuwa ukimwandikia wahy Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo hakikisha unaipatiliza Qur-aan na kuikusanya.”[2]
[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (868).
[2] al-Bukhaariy (4986).
Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 120
Imechapishwa: 22/09/2026
https://firqatunnajia.com/fadhilah-za-zayd-bin-thaabit/