184 – Muhammad bin Yahyaa bin Muhammad ametukhabarisha: Ahmad bin ´Abdillaah bin Abiy Shu´ayb ametukhabarisha: al-Haarith bin ´Umayr amenihadithia: Ayyuub ametukhabarisha, kutoka kwa Naafiy´, ambaye ameeleza:

“Ibn ´Umar aliota kana kwamba ana kipande cha kijitabu mkononi mwake na haashiri nacho chochote Peponi isipokuwa kinamrukia. Akamsimulia ndoto hiyo Hafswah, ambaye naye akamweleza nayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ambaye alisema: “´Abdullaah bin ´Umar ni mtu mwema.”[1]

[1] al-Bukhaariy (3740) na Muslim (2478).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 121
  • Imechapishwa: 22/09/2026