187 – Muhammad bin al-Muthannaa ametukhabarisha: Khaalid ametukhabarisha, kutoka kwa Humayd, kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimtembelea Ummu Sulaym, ambaye akampa tende na siagi. Akasema: “Rudisha mafuta yako ya siagi kwenye chombo chake na tende zako kwenye bakuli lake. Kwa sababu nimefunga.” Kisha akaenda kwenye kona ya nyumba, akaswali swalah isiyokuwa ya faradhi na akamuombea du´aa Ummu Sulaym na watu wa nyumbani kwake. Ummu Sulaym akasema: “Ee Mtume wa Allaah, nataka kukuomba kitu.” Akasema: ”Kipi?” Akasema: ”Anas ni mtumishi wako.” Hakuacha kheri yoyote miongoni mwa kheri za Aakhirah wala kheri za ulimwenguni isipokuwa aniliombea nayo. Kisha akasema: “Ee Allaah! Mruzuku mali na watoto na umbariki kwavyo.” Mimi ni miongoni mwa Answaar waliokuwa na mali nyingi. Binti yangu amenieleza kwamba vizazi vyangu mia moja na ishirini walizikwa kabla ya al-Hajjaaj kufika Baswrah.”[1]

188 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Ja´far bin Sulaymaan ametukhabarisha, kutoka kwa al-Ja´d Abu ´Uthmaan: Anas bin Maalik ametukhabarisha:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipita ambapo Umm Sulaym akasikia sauti yake na akasema: “Wazazi wangu watolewe kwako fidia, ee Mtume wa Allaah! Anas kijidogo!” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akaniombea du´aa tatu. Nimeshaona mbili katika hizo na nataraji ya tatu huko Aakhirah.”[2]

[1] al-Bukhaariy (1982) na Muslim (2481).

[2] Muslim (2481).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 122-123
  • Imechapishwa: 23/09/2026