185 – Muhammad bin al-Muthannaa ametukhabarisha: Khaalid ametukhabarisha: Humayd ametuhadithia, kutoka kwa Anas, ambaye amesema:

“ar-Rabiy’ alivunja jino la mbele la kijakazi ambapo wakaomba msamaha wao. Wakakataa na wakadhihirisha fidia. Wakaja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ambaye aliamrisha kulipiza kisasi. Amesema Anas bin an-Nadhwr: “Ee Mtume wa Allaah! Hivi kweli livunjwe jino la mbele la ar-Rabiy´? Naapa kwa Yule aliyekutuma kwa haki, hawatolivunja!” Akasema: ”Ee Anas, Kitabu cha Allaah kinasema kulipiza kisasi.” Ndipo watu wale wakakubali kusamehe ambapo akasema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Allaah anao waja ambao wanapoapa kwa Allaah, basi Anawaitikia.”[1]

186 – Muhammad bin Haatim bin Nu´aym ametukhabarisha: Hibbaan ametukhabarisha: ´Abdullaah ametukhabarisha, kutoka kwa Sulaymaan bin al-Mughiyrah, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambaye amesema:

”Ami yangu Anas, ambaye nilipewa jina lake, hakushuhudia Badr pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Likamkuwia kubwa hilo na akasema: “Vita vya kwanza ambavyo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameshuhudia nimevikosa? Kama Allaah atanikutanisha na vita vingine pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi Allaah ataona nitachofanya.” Aliogopa kusema kitu kingine. Mwaka uliofuata akashiriki vita vya Uhud pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Sa´d bin Mu´aadh akamgeukia na kusema: “Ee Abu ´Amr, unaenda wapi?” Akasema: ”Nahisi harufu ya Pepo inatoka kwenye Uhud.” Akapigana mpaka alipouliwa. Wakapata mwilini mwake kuna alama za madonda themanini katika mwili wake. Shangazi yangu dada yake ar-Rabiy’ bint an-Nadhwr akasema: ’’Sikumtambua ndugu yangu isipokuwa tu kwa vidole vyake.” Hapo ndipo kuliteremshwa Aayah isemayo:

مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ ۖ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ ۖ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا

”Miongoni mwa waumini wapo wanaume waliotimiza kikweli waliyoahidiana na Allaah. Basi miongoni mwao wako waliotimiza nadhiri yao na wengine  wanasubiri – na hawakubadilisha hata kidogo.”[2]

[1] al-Bukhaariy (4611) na Muslim (1675).

[2] 33:23 al-Bukhaariy (2805) na Muslim (1903).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 121-122
  • Imechapishwa: 23/09/2026