Eti TV nyumbani kwa ajili ya taarifa ya khabari

Swali la tano: Ni ipi hukumu ya kuweka TV [nyumbani]?

Jibu: Ninachowanasihi ndugu zangu waache kuweka TV kabisa. Haijalishi kitu hoja itayotolewa kwa sababu hii leo madhara yake yamekuwa ni makubwa kuliko manufaa yake.

Swali la tano: Kuna wanaosema kuwa wanaweka kwa sababu ya kusikiliza taarifa ya khabari.

Jibu: Mtu mwenye akili hatakiwi kuiweka nyumbani kwake japokuwa itakuwa ni kwa sababu ya taarifa ya khabari. Kwa sababu akiiweka nyumbani kwa ajili ya kutazama taarifa ya khabari hatokomekana na kutosheka na kutazama taarifa ya khabari peke yake. Ni lazima atatazama taarifa ya khabari na mengineyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=90775
  • Imechapishwa: 07/10/2018