Swali: Najaribu kuja katika elimu na wewe unastahiki kujiwa. Lakini, ee Shaykh wetu, wazazi wangu wamekuwa wazee na sisi tuna wanawake na nyumba iko mbali na chuo kikuu hichi. Nafsi zetu zinachoka kuja na wewe uko na kiigizo kutoka kwa Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na as-Salaf as-Swaalih ambapo walikuwa wakienda huku na kule kwa ajili ya kulingania katika dini ya Allaah, jambo ambalo wafanya na unazunguka. Lakini kuhusu mikutano hii unaweza kuzunguka huku na kule katika nyakati mbalimbali ukavizungukia vyuo vikuu vingi vilivyoko nchini baada ya darsa kusimama. Hakika sisi tunafarijika juu ya hayo. Usiseme kuwa kusikiliza kwenye kanda kunatosha. Kwani mwenye kujionea mwenyewe si sawa na mwenye kusikiliza.
Jibu: Amezisoma fikira zangu muulizaji huyu. Mimi nilikuwa najiambia ndani ya nafsi kwamba nakujieni na nahudhuria kwenu kupitia kaseti. Lakini naona kuwa mtu huyu amezisoma fikira zangu. Hapana shaka kwamba halinganizi mwenye kusikiliza na mwenye kuona. Lakini akitumia hoja dhidi yangu juu ya kanda au maneno, basi na mimi namwambia kwamba elimu inaendewa na wala haimfuati mtu. Lakini ni kweli kwamba tuna kiigizo chema kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna mwanamke mmoja alimwambia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ee Mtume wa Allaah! Wanaume wametushinda. Tufanyie siku moja uwe ukitupitia.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaahidi siku moja ambapo akiwaendea, akiwapa mawaidha na kuwakumbusha.
Mimi nadhani kuwa hii leo miji – na himdi zote ni za Allaah – imekaribiana. Kumekuwa na magari n.k. Mambo yamekuwa mepesi. Tarajia malipo kutoka kwa Allaah na hudhuria katika elimu. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Atakayechukua njia akitafuta ndani yake elimu, basi Allaah atamfanyia wepesi njia ya kuielekea Pepo.”
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/806
- Imechapishwa: 25/03/2018

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/806
Imechapishwa: 25/03/2018
https://firqatunnajia.com/elimu-inafuatwa-na-haimfati-mtu-2/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)