“Ee Allaah tubarikie katika Rajab na Sha’baan na utufikishe Ramadhaan”

Swali: Baadhi ya watu hufunga baadhi ya siku za Rajab wakitoa dalili kwa Hadiyth isemayo:

اللهم بارك لنا في رجب، وشعبان، وبلغنا رمضان

“Ee Allaah tubarikie katika Rajab na Sha’baan na utufikishe Ramadhaan.”

Ni upi usahihi wa Hadiyth hii?

Jibu: Hadiyth hiyo ni dhaifu, si Swahiyh na haina hoja.

“Ee Allaah tubarikie katika Rajab… ”

haina dalili ya kuifanya Rajab itengewe ´ibaadah maalumu. Zaidi ya hayo Hadiyth yenyewe ni dhaifu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2757/درجة-حديث-اللهم-بارك-لنا-في-رجب-وشعبان
  • Imechapishwa: 14/02/2026