Swali: Je, duyuthi ni mtu anayemruhusu mke wake kuangalia mambo ya ufisadi kwenye TV au video, anayemruhusu atoke akiwa ni mwenye kuonyesha mapambo au duyuthi ni yule anayekubali mke wake kuziniwa? Ni lini inasemwa kuwa mwanaume ni duyuthi wa kweli?

Jibu: Kinachotambulika ni kwamba duyuthi ni mwanaume anayekubali kufanyika kwa machafu na ufisadi kwa familia yake. Ni yule anayekubali au kuridhia mke wake au jamaa zake kufanya mambo machafu, kama uzinzi au vitendo vingine vichafu. Huyu ndiye anayestahili kuitwa duyuthi kwa sababu anakubali maasi na uovu kufanywa katika nyumba yake na wakati mwingine anaweza hata kuyahamasisha au kupata pesa kupitia hayo. Lakini pia kumruhusu mke au watu wa nyumbani kuingia katika mambo yanayopelekea kwenye uzinzi, kama kuona wanaume uchi, kusikiliza nyimbo na muziki au vyombo vya uovu, ni njia inayoelekea kwenye uduyuthi na ufisadi. Haya siyo duyuthi yenyewe moja kwa moja, bali ni mambo yanayoweza kumfikisha mtu kwenye hali hiyo.

Swali: Je, duyuthi ameharamishiwa Pepo?

Jibu: Ni jambo limepokelewa katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunamuomba Allaah usalama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1199/تعريف-الديوث-وحكمه
  • Imechapishwa: 06/02/2026