Swali: Je, ni lazima kusoma du´aa ya kufungulia swalah katika swalah ya kumswalia maiti?

Jibu: Swalah ya kumswalia maiti ni swalah iliyowepesishwa. Wanazuoni wameeleza kuwa haisomwi du´aa ya kufungulia swalah ndani yake. Badala yake mtu aanze kwa kuomba kinga dhidi ya shaytwaan, Basmalah na asome Suurah ”al-Faatihah”. Hahitaji kusoma du´aa ya kufungulia swalah, kwa sababu ni swalah iliyowepesishwa na inahitajika kuharakishwa ili kumharakisha maiti. Kwa hiyo kilicho bora ni kutosoma du´aa ya kufungulia. Hivi ndivyo ilivyotajwa na wanazuoni. Wengine katika wanazuoni wanaona kuwa du´aa ya kufungulia inajuzu kusomwa, lakini maoni ya karibu zaidi na usawa – na Allaah ndiye ajuaye zaidi – ni kutosoma. Kwa sababu hii ni swalah iliyofupishwa isiyo na Rukuu´ wala Sujuud.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1159/حكم-دعاء-الاستفتاح-في-صلاة-الجنازة
  • Imechapishwa: 02/01/2026