Inafaa kuzidisha juu ya yale yaliyothibiti katika du´aa ya Qunuut?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzidisha katika du´aa ya Qunuut juu ya yale yaliyothibiti ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza al-Hasan bin ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhumaa)?

Jibu: Kuongeza juu ya hilo hakuna neno. Kwa sababu ikithibiti kuwa sehemu hii ya du´aa na du´aa hii haikuwekewa mpaka unaokataza kuongeza juu yake msingi ni kwamba mtu anaomba kwa kile anachokitaka. Lakini baada ya kusoma kile kilichothibiti, au kwa msemo mwingine inatakiwa kutanguliza kile kilichothibiti, baada ya hapo yule anayetaka kuzidisha hakuna neno. Kwa ajili hii imethibiti kuwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) waliwalaani makafiri katika Qunuut yao pamoja na kuwa haya hayakuthibiti katika yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza al-Hasan bin ´Aliy bin Abiy Twaalib. Hapo kutakuwa hakuna utatizi wowote katika masuala haya. Pamoja na kuwa matamshi ya Hadiyth:

“Alinifunza du´aa nitayoomba nayo katika Qunuut ya Witr.”[1]

mtu anaweza kusema kuwa udhahiri wake unaonyesha kuwa kuna du´aa zengine mbali na hiyo. Kwa sababu amesema:

“… du´aa nitayoomba nayo katika Qunuut ya Witr.”

Kwa hali yoyote jibu ni kwamba kuongeza juu ya hiyo hakuna ubaya wowote. Muislamu anatakiwa kuomba kwa du´aa zilizoenea muhimu kwa waislamu katika dini na dunia yao.

[1] Abu Daawuud na wengineo

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/137)
  • Imechapishwa: 18/06/2017