Swali 658: Je, inajuzu kuomba kwa du´aa ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh):

اللهم إن كنت كتبتني شقيًا فامحه، واكتبني سعيدًا

“Ee Allaah, ikiwa umeniandika miongoni mwa watu waliopotea ifute na uniandike miongoni mwa watu wa furaha”?[1]

Jibu: Dhahiri yake ni kuwa haifa. Bora ni kutofanya hivo.

[1] Ameipokea Ibn Jariyr katika ”Tafsiyr” yake (13/563) kuhusiana na Aayah ya ar-Ra´d:

يَمْحُو اللَّـهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُ أُمُّ الْكِتَابِ

“Allaah anafuta yale ayatakayo na anathibitisha na Kwake ndiko kuna Mama wa Kitabu.” (39:11)

kupitia kwa Abu Hakiymah, kutoka kwa Abu ´Uthmaan an-Nahdiy, kutoka kwake. Cheni yake ya wapokezi haina neno. Abu Haatim amesema kuhusu Abu Hakiymah katika ”al-Jarh” (7/20):

”Hadhi yake ni ya kuaminika.”

Vilevile tazama ”Tabswir-ul-Muntabiyhiy” (1/405) na ”al-Istighnaa´” cha Ibn ´Abdil-Barr (1/589). Imepokelewa pia riwaya mfano wa hiyo kutoka kwa Ibn Mas’uud.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 239
  • Imechapishwa: 21/06/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´