Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muislamu ni ndugu ya muislamu mwenzie.”

Hii leo waislamu wengi wamewasahau ndugu zao sehemu kote ulimwenguni. Wamesahau kufanya kitu kichache ambacho wanaweza kufanya; nacho ni kuwaombea du´aa au kuwasaidia kwa kile kilichozidi juu ya haja zao. Tunaomba uwape nasaha au kalima yenye kunufaisha inayoweza kuwatikisa wale waliohudhuria au kuamsha hisia zao.

Jibu: Hapana shaka kwamba zama zetu hizi ni zama za fitina na shari isipokuwa wale waliolindwa na Allaah. Tukizingatia yale yaliyo pambizoni mwetu basi tutaona mambo mengi kukiwemo mauji, ukatili na khofu. Vilevile tunasikia mambo ambayo tunamuomba Allaah atulinde nayo na awaondolee nayo ndugu zetu.

Lililo la wajibu kwetu kwa ndugu kabla ya kila kitu zetu ni kuwaombea uthabiti na kuwaombea kutoka kwa Allaah msaada, kwamba awasaidie kwa yale aliyowajaribu, kuwakirimu kwa kitu ambacho Allaah (´Azza wa Jall) atakuwa amesahilisha kila mmoja kwa kiasi cha hali yake. Lakini ni wajibu kwetu kujua ya kwamba kuna ambao wako pambizoni mwetu ambao wako katika haja kubwa na hawako mbali na sisi. Wao pia wanahitajia kusaidiwa:

“Muumini kwa muumini mwenzake ni kama jengo; upande mmoja unaupa nguvu upande mwingine.”

Hakuna dogo kuliko kuwaombea kwa Allaah, kama alivyosema muulizaji, uthabiti, nusura na awafanye kushinda maadui wao ambao kiuhalisia ni maadui wa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (39) http://binothaimeen.net/content/892
  • Imechapishwa: 15/08/2018