Himdi zote anastahiki Allaah. Tunamhimidi Yeye, kumuomba msaada na msamaha. Tunajilinda kwa Allaah kutokamana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yule mwenye kuongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na yule mwenye kupotezwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Ninashuhudia ya kwamba hapana mola wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa ni mmoja asiyekuwa na mshirika, na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa nyinyi ni waislamu.” (03:102)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni kutokana na nafsi moja na akaumba kutoka humo mke wake na akaeneza kutoka hao wawili wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Allaah ambaye Kwake mnaombana na jamaa. Hakika Allaah amekuwa juu yenu ni Mwenye kuchunga.” (04:01)

ا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا

“Enyi mlaomini! Mcheni Allaah na semeni kauli nyofu ya haki. Atakutengenezeeni „amali zenu na atakusameheni madhambi yenu; na anayemtii Allaah na Mtume Wake, basi kwa yakini amefanikiwa mafaniko makuu.” (33:70-71)

Amma ba´d:

Hakika maneno bora ni Kitabu cha Allaah na uongofu kabisa ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Uovu wa mambo ni yale ya kuzua. Kila kitakachozushwa ni Bid´ah. Kila Bid´ah ni upotevu. Kila upotevu ni Motoni.

Amma ba´d:

Hiki ni kijitabu kifupi kinachozungumzia dalili za Tawhiyd nimekipa jina “alQawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd”. Nimekusanya dalili zake kutoka katika Qur-aan tukufu na zile Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zilizothibiti. Chapa ya kwanza ilichapwa Hudaydah 1430. Hivi tena ninawawakilishia waheshimiwa wasomaji chapa ya pili. Katika chapa hii kuna nyongeza na ukaguzi fulani. Ninamuomba Allaah mtukufu anufaishe kwacho na ajaalie matendo yangu yote yawe kwa ajili Yake Pekee. Hakika Yeye juu ya kila kitu ni muweza.

Swalah na salaam na baraka zimwendee mja na Mtume Wake Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake mpaka siku ya Qiyaamah. Himdi zote ni za Allaah, Mola wa walimwengu.

23 Jumaada al-Uwlaa 1406, Swan´aa’

Abu Ibraahiym Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab bin ´Aliy al-Wasswaabiy al-´Abdaliy

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qawl al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd
  • Imechapishwa: 05/08/2020