Swali: Je, ni Sunnah kuchelewesha Dhuhr kwa ambaye anaswali peke yake na mwanamke?

Jibu: Kuchelewesha Dhuhr kwa sababu ya joto kali linawahusu watu wote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika joto kali unatokamana na mvuke wa Jahannam. Kukiwa na joto kali basi  pateni baridi kwa swalah.”[1]

Hadiyth inawazungumzisha watu wote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakujengea sababu kwa uzito wa kwenda msikitini wakati wa joto kali, bali kwamba joto kali unatokamana na mvuke wa Jahannam. Joto kali linampata anayeenda msikitini na anayeswali peke yake. Mpaka wanawake wanaguswa na jambo hilo na hivyo inapendeza kwao kuchelewesha Dhuhr wakati wa joto kali.

[1] al-Bukhaariy (535).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/205)
  • Imechapishwa: 19/05/2026