Swali: Je, swalah ni sahihi ya ambaye anaswali Dhuhr nyuma ya anayeswali ´Aswr?
Jibu: Hapana vibaya. Swalah yake ni sahihi kwa mujibu wa maoni yenye nguvu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika si vyenginevyo kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”[1]
Hakukuthibiti kitu kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kinachofahamisha kuwa ni lazima nia ya imamu na maamuma ziendane sambamba. Kwa hivyo kila mmoja analipwa kutegemea na nia yake, kama inavyojulisha Hadiyth hii:
“… na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”
[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/445)
- Imechapishwa: 19/04/2026
Swali: Je, swalah ni sahihi ya ambaye anaswali Dhuhr nyuma ya anayeswali ´Aswr?
Jibu: Hapana vibaya. Swalah yake ni sahihi kwa mujibu wa maoni yenye nguvu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika si vyenginevyo kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”[1]
Hakukuthibiti kitu kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kinachofahamisha kuwa ni lazima nia ya imamu na maamuma ziendane sambamba. Kwa hivyo kila mmoja analipwa kutegemea na nia yake, kama inavyojulisha Hadiyth hii:
“… na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”
[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/445)
Imechapishwa: 19/04/2026
https://firqatunnajia.com/dhuhr-nyuma-ya-imamu-anayeswali-aswr/