Amegundua kuwa alitakikana kuoga kabla ya kuswali

Swali: Vipi kuhusu ambaye ameswali na baada ya kuswali ikabaini kuwa ni mwenye hadathi kubwa inayomuwajibishia kuoga?

Jibu: Kila mtu ambaye ameswali kisha baada ya kuswali ikambainikia kuwa alikuwa na hadathi kubwa au hadathi ndogo, basi ni wajibu kwake kujitwahirisha kutokana na hadathi hii na kuirudia swalah yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah haikubali swalah pasi na twahara.”[1]

[1] Muslim (224).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/370-371)
  • Imechapishwa: 19/04/2026