Swali: Ni Dhikr ipi bora zaidi?

Jibu:

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ni Wake ufalme na ni Zake himdi zote njema, Naye juu ya kila jambo ni muweza.”

pamoja na Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah ni manne:

سبحان الله، والحمد لله، ولا إله إلا الله، والله أكبر

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote ni Zake, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa.”,

Amesema:

”Mema yenye kubaki ni:

سبحان الله، والحمد لله، ولا إله إلا الله، والله أكبر، ولا حول ولا قوة إلا بالله

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu, himdi zote ni Zake, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Lakini Dhikr iwe kwa moyo, kwa kwa viungo vya mwili pamoja na kumtii Allaah na kuacha kumuasi.

Swali: Vipi ikiwa mtu siku nzima atasema tu:

ولا إله إلا الله

”Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah.”?

Jibu: Hilo ni jambo jema. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Atakayesema:

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ni Wake ufalme na ni Zake himdi zote njema, Naye juu ya kila jambo ni muweza.”

mara mia kwa siku, basi atakuwa na thawabu sawa na kuacha huru watumwa kumi, ataandikiwa mema mia moja, atafutiwa makosa mia moja moja, atakuwa na kinga dhidi ya shaytwaan kwa siku hiyo hadi kuingie jioni na hakuna atakayekuja na kitu bora kuliko alichokuja nacho yeye isipokuwa tu yule aliyefanya zaidi ya hivo.”[1][2]

Kwa hiyo mja amtaje Allaah kwa wingi. Akikusanya pamoja Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr; basi itakuwa kamilifu zaidi.

[1] al-Bukhaariy (6403) na Muslim (2691).

[2] Maana yake imekwishatangulia katika Hadiyth (08).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31198/ما-افضل-الذكر
  • Imechapishwa: 12/10/2025