Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

37- Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema kutokana na yale aliyoyapokea kutoka kwa Mola Wake, hali ya kuwa ni Mwenye kutukuka, ya kwamba amesema:

“… akiazimia [kufanya tendo ovu] na mwishowe akalifanya, Allaah atamwandikia tendo ovu moja.”

Hii ni Rahmah kubwa ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa waja Wake waumini: ya kwamba wakifanya ovu hawaongezewi dhambi hiyo, bali Allaah Anawaandikia tendo ovu moja. Kinyume na mwenye kutenda tendo jema anaongezewa [mara kumi hadi mara mia saba na zaidi ya hivo]. Kwa ajili hii hatoangamia siku ya Qiyaamah isipokuwa yule mwenye kustahiki kuangamia kweli.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 505
  • Imechapishwa: 10/05/2020