Hakika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemdhamini yule mwenye kushikamana na Qur-aan na Sunnah uongofu, uokozi na kutopotea, mambo ambayo yanapelekea katika kuangamia duniani na majuto Aakhirah. Kadhalika amekataza kuzua katika dini ya Allaah na akatahadharisha Bid´ah na akaubainishia Ummah wake ya kwamba kila Bid´ah itayofanywa katika dini ya Allaah ni upotevu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth iliyosimuliwa na al-´Irbaadhw bin Saariyah pale aliposema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutolea mawaidha mazito yaliyozitikisa nyoyo zetu na yakafanya machozi kututiririka. Tukamwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Kana kwamba ni mawaidha ya kutuaga. Tuusie!” Akasema: “Ninakuusieni kumcha Allaah na usikivu na utiifu hata kama mtaongozwa na mja. Hakika yule atayeishi katika nyinyi basi atakuja kuona upotevu mkubwa. Hivyo basi, jilazimieni na Sunnah zangu na Sunanh za makhaliyfah wangu waongofu. Ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo ya kuzua. Hakika kila Bid´ah ni upotevu.”[1]

[1] Abu Daawuud (4443) na at-Tirmidhiy (2815).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bid´ah – Dhwawaabitwuhaa wa atharuhaa as-Sayyiu´ fiyl-Ummah, uk. 09
  • Imechapishwa: 27/08/2020