Swali: Walinganizi wamekuwa wengi leo lakini hata hivyo ni wachache katika wao wanaolingania katika Tawhiyd na ´Aqiydah. Je, asiyelingania katika Tawhiyd anazingatiwa kuwa anaenda kinyume na Mitume na hivyo kutahadharishwe juu ya Da´wah yake?
Jibu: Ndio, kutahadharishwe. Asiyelingania katika Tawhiyd na anasema kuwa Tawhiyd sio lazima. Badala yake kutahadharishwe madhambi, maasi, ribaa, zinaa na mfano wa hayo, hii ni Da´wah isiyokuwa na kichwa. Ni kama mfano wa mwili usiokuwa na kichwa. Kuna mwili usiokuwa na kichwa ukawa hai? Hapana. Ni maiti. Hii ni Da´wah maiti ambayo hakuna faida nyuma yake. Da´wah hii inaenda kinyume na Da´wah ya Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam). Kitu cha kwanza walichokuwa wakianza nacho ni Tawhiyd. Tawhiyd ikithibiti na kuhakikishwa ndio sasa wanawafunza watu mambo ya dini yao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh):
“Iwe kitu cha kwanza utacholingania kwacho “Kuhushudia ya kwamba mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Wakikuitikia katika hilo wafunze kuwa Allaah amewafaradhishia swalah tano mchana na usiku… “
Wasipomuitikia Tawhiyd hakuna faida ya hayo mengine. Lau wataswali usiku na mchana swalah zao hazina faida yoyote.
Kila Da´wah isiyotilia umuhimu Tawhiyd basi hiyo ni Da´wah maiti na haizalishi kitu kamwe.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (16) http://alfawzan.af.org.sa/node/2109
- Imechapishwa: 05/07/2020
Swali: Walinganizi wamekuwa wengi leo lakini hata hivyo ni wachache katika wao wanaolingania katika Tawhiyd na ´Aqiydah. Je, asiyelingania katika Tawhiyd anazingatiwa kuwa anaenda kinyume na Mitume na hivyo kutahadharishwe juu ya Da´wah yake?
Jibu: Ndio, kutahadharishwe. Asiyelingania katika Tawhiyd na anasema kuwa Tawhiyd sio lazima. Badala yake kutahadharishwe madhambi, maasi, ribaa, zinaa na mfano wa hayo, hii ni Da´wah isiyokuwa na kichwa. Ni kama mfano wa mwili usiokuwa na kichwa. Kuna mwili usiokuwa na kichwa ukawa hai? Hapana. Ni maiti. Hii ni Da´wah maiti ambayo hakuna faida nyuma yake. Da´wah hii inaenda kinyume na Da´wah ya Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam). Kitu cha kwanza walichokuwa wakianza nacho ni Tawhiyd. Tawhiyd ikithibiti na kuhakikishwa ndio sasa wanawafunza watu mambo ya dini yao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh):
“Iwe kitu cha kwanza utacholingania kwacho “Kuhushudia ya kwamba mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Wakikuitikia katika hilo wafunze kuwa Allaah amewafaradhishia swalah tano mchana na usiku… ”
Wasipomuitikia Tawhiyd hakuna faida ya hayo mengine. Lau wataswali usiku na mchana swalah zao hazina faida yoyote.
Kila Da´wah isiyotilia umuhimu Tawhiyd basi hiyo ni Da´wah maiti na haizalishi kitu kamwe.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (16) http://alfawzan.af.org.sa/node/2109
Imechapishwa: 05/07/2020
https://firqatunnajia.com/dawah-maiti-%e2%80%82/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)