10. Dawa za matone ya macho mchana wa Ramadhaan zinafunguza?

Swali: Dawa za matone ya macho mchana wa Ramadhaan zinafunguza?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba dawa za matone ya macho hazifunguzi. Ingawa kuna tofauti kati ya wanachuoni. Wako waliosema kuwa akihisi ladha kooni basi anafungua. Maoni sahihi ni kwamba hazifunguzi kabisa. Kwa sababu macho sio maeneo ya kupitishia chakula. Lakini endapo atasimama upande wa salama zaidi na akalipa kwa ajili ya kutoka nje ya tofauti basi hakuna neno. Ambaye atahisi ladha kooni mwake hakuna neno. Vinginevyo maoni yenye nguvu ni kwamba hayafunguzi. Ni mamoja amehisi ndani ya macho au ndani ya masikio.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 10-11
  • Imechapishwa: 31/03/2021