Dalili wanayotumia waabudia makaburi

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمً ا

“Hatukutuma Mtume yeyote isipokuwa atiiwe kwa idhini ya Allaah. Na lau wao pale walipojidhulumu nafsi zao wangelikujia wakamuomba Allaah msamaha na Mtume akawaombea msamaha, basi wangelimkuta Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.”[1]

Wanaoabudu makaburi na kuyaomba msamaha wametumia Aayah hii. Wamesema ni kwa sababu Allaah amesema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمً ا

“Na lau wao pale walipojidhulumu nafsi zao wangelikujia wakamuomba Allaah msamaha na Mtume akawaombea msamaha, basi wangelimkuta Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.”

Unapofanya dhambi eti nenda katika kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuomba msamaha na Mtume atakusamehe. Watu hawa wamepotea upotevu wa mbali kabisa. Aayah imeweka wazi kabisa. Imesema:

إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ

“… walipojidhulumu nafsi zao… ”

Aayah haikusema:

“Watapozidhulumu nafsi zao wangelikujia.”

Aayah inaelezea juu ya kitu kimechopita ambapo wamezidhulumu nafsi zao kutokana na waliyofanya kisha wakakujia pindi uko hai na wakamuomba Allaah msamaha na wewe, basi wangelimkuta Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. Ama kuhusu baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufa hawezi akamsamehe yoyote. Kwa kuwa matendo yake yamekatika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapokufa mwanaadamu matendo yake [yote] hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika kwayo au mtoto mwema mwenye kumuombea.”[2]

[1] 04:64-65

[2] Muslim (1631).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/257-258)
  • Imechapishwa: 01/12/2024