Swali: Ikiwa utoko huu unachengua wudhuu´ unapotoka mwingi ni kwa nini basi hakukuonekana dalili ya wazi inayobainisha hali hii wakati wa Maswahabah wa kike kwa sababu utoko huu hutoka kwa sifa ya kuendelea na ni jambo linalowatokea wanawake wengi.
Jibu: Uhakika wa mambo ni kwamba tatizo hili alilotaja muulizaji ni la kweli. Kwa sababu utoko huu unaotoka ni mtihani unaowatokea wanawake wengi. Lakini baada ya utafiti wa kutosha sikumpata mwanachuoni yeyote anayesema kuwa hauchengui wudhuu´ isipokuwa mwanachuoni mmoja tu, naye si mwengine ni Ibn Hazm. Hakuna mwanachuoni yeyote kabla yake aliyesema hivo ili tuweze kusema kuwa Salaf wa Ummah wamesema kuwa utoko hauchengui wudhuu´.
Mimi hivi sasa nasema ya kwamba akipatikana Salaf yeyote wa Ummah huu mwenye kuonelea ya kwamba utoko huu hauchengui wudhuu´ basi maoni yake yako karibu zaidi na usawa kuliko maoni yanayosema kuwa unachengua. Mosi ni kwa sababu ya ule uzito unaopatikana ndani yake. Pili ni kwa sababu hili ni jambo la kawaida. Sio hadathi ya kilazima kama mwanamke anayetokwa na damu ya ugonjwa. Bali ni jambo la kawaida kwa wanawake wengi. Kwa hivyo mkimpata Salaf yeyote wa Ummah huu mwenye kuonelea ya kwamba utoko huu hauchengui wudhuu´ basi maoni yake yako karibu zaidi na usawa. Msipopata basi si haki kwetu kutoka katika maafikiano ya Ummah.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (30)
- Imechapishwa: 23/10/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)