Swali: Maneno Yake Allaah aliposema:

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ

”Ni nani aliyepotea zaidi kuliko yule anayemwomba badala ya Allaah, ambao hatowaitikia mpaka siku ya Qiyaamah nao hawatambui maombi yao. Na [Qiyaamah] watakapokusanywa watu [miungu ya uongo] watakuwa maadui wao na watakuwa kwa ‘ibaadah zao ni wenye kuzikanusha.”[1]

Je, hapa kuna dalili ya kwamba wafu hawasikii?

Jibu: Ndio, hawasikii. Aayah iko wazi:

إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ

”Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu.”[2]

[1] 46:5-6

[2] 35:14

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24550/تفسير-قوله-تعالى-وهم-عن-دعاىهم-غافلون
  • Imechapishwa: 31/10/2024