Daima mume anaswali na mke baada ya kurejea kutoka msikitini

Swali: Mara nyingi mtu huyu huja nyumbani kwake baada ya swalah na kuswali pamoja na mke wake Rak´ah mbili, ambazo kwake ni Raatibah, na kwa mke wake ni faradhi. Lakini watu wengine wamemkemea na kusema kwamba swalah ya mkusanyiko katika swalah zinazopendeza haikuthibitika isipokuwa mara chache na kwamba asifanye hivo mara nyigni. Je, maoni yako ni yapi kuhusu hili?

Jibu: Kuacha jambo hili ni bora zaidi, kwa sababu hili halikufanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye kuswali Raatibah peke yake na mkewe anaswali peke yake ndiyo lililo bora, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapokuja nyumbani kwake huswali Raatibah peke yake na wanawake wanaswali swalah zao za faradhi peke yao. Hili ndilo lililo bora. Hata hivyo ikiwa ataswali pamoja naye, yeye akiwa anaswali faradhi na mume akiwa katika Sunnah, swalah hiyo inasihi, kama ilivyosihi Mu´aadh alipowaswalisha Maswahabah wake. Katika hali hyio yeye inakuwa Sunnah na wao faradhi. Pia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali swalah ya khofu pamoja na kikundi cha pili Rak´ah mbili, yeye akiwa katika Sunnah na wao katika faradhi. Hivyo basi hakuna tatizo. Lakini ni bora zaidi kwa mwanamke kuswali peke yake na mume kuswali Raatibah peke yake, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hili ndilo lililo bora.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25138/حكم-اىتمام-الزوجة-لفريضتها-براتبة-زوجها
  • Imechapishwa: 13/02/2025