Dai haki yako kwa njia nyingine, si rushwa

Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa rushwa iwapo haki yangu inayotambulika au fidia yangu iliyoamuliwa haitapatikana isipokuwa kwa njia ya rushwa?

Jibu: Haijuzu kutoa rushwa, kwa kuwa kufanya hivo maana yake ni kusaidia katika batili. Kusaidia kupoteza haki na kuwadhulumu watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah amemlaani mwenye kutoa rushwa na mwenye kupokea.”

Vilevile mpatanishi kati yao pia. Hivyo haijuzu kushirikiana katika batili na maasi. Bali dai haki yako kwa njia ya Kishari´ah. Ikiwa kuna mtu anakuzuia, peleka jambo lake kwa wenye mamlaka na umuanike kwa uzembe wake. Usimsaidie katika maasi ya Allaah kwa hongo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30098/حكم-الرشوة-لمن-لا-يمكنه-تحصيل-حقه-الا-بها
  • Imechapishwa: 07/09/2025