Swali: Mwanamke anasema kuwa mama yake amefariki na amemwacha yeye na dada yake wa baba na mama mmoja. Pia kuna watoto watatu: ndugu wa mama yake wa upande wa baba, mama yake na dada yao. Ni ipi hukumu?
Jibu: Ikiwa hali halisi ni kama ulivyotaja, basi mali iliyoachwa na mama yako (Rahimaha Allaah) itagawanywa kati yako na dada yake kwa nusu kwa nusu. Watoto wa ndugu yake hawapati kitu katika urithi, kwa sababu dada yake katika suala kama hili huwazuia watoto wa ndugu kupata mirathi. Ikiwa mama yako aliacha wasia kwa jambo fulani, basi wasia wake hutangulizwa kabla ya kugawanywa urithi kati yako na dada yake, ikiwa wasia huo ni theluthi au chini yake kwa mujibu wa Shari´ah. Ikiwa alikuwa na deni lililothibiti, basi anza kwanza kulipa deni lake kabla ya kutekeleza wasia na kabla ya kugawanya mirathi kati yako na dada yake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/195)
- Imechapishwa: 16/03/2026
Swali: Mwanamke anasema kuwa mama yake amefariki na amemwacha yeye na dada yake wa baba na mama mmoja. Pia kuna watoto watatu: ndugu wa mama yake wa upande wa baba, mama yake na dada yao. Ni ipi hukumu?
Jibu: Ikiwa hali halisi ni kama ulivyotaja, basi mali iliyoachwa na mama yako (Rahimaha Allaah) itagawanywa kati yako na dada yake kwa nusu kwa nusu. Watoto wa ndugu yake hawapati kitu katika urithi, kwa sababu dada yake katika suala kama hili huwazuia watoto wa ndugu kupata mirathi. Ikiwa mama yako aliacha wasia kwa jambo fulani, basi wasia wake hutangulizwa kabla ya kugawanywa urithi kati yako na dada yake, ikiwa wasia huo ni theluthi au chini yake kwa mujibu wa Shari´ah. Ikiwa alikuwa na deni lililothibiti, basi anza kwanza kulipa deni lake kabla ya kutekeleza wasia na kabla ya kugawanya mirathi kati yako na dada yake.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/195)
Imechapishwa: 16/03/2026
https://firqatunnajia.com/dada-anawazuia-watoto-wa-ndugu-yake-kurithi/