Chupi ya mwenye ugonjwa wa kutokwa na mkojo mara kwa mara

Swali: Je, ni wajibu kwa mtu ambaye ana ugonjwa wa kutokwa hovyo na mkojo kuvua chupi?

Jibu: Mwenye ugonjwa wa kutokwa hovyo achunge muda wa swalah ya faradhi na aswali kulingana na hali yake. Atawadha baada ya kuingia wakati wa swalah na aswali kulingana na hali yake. Atambe kwa maji na kisha aswali kulingana na hali yake, hata kama kitu kitamtoka wakati wa swalah. Lakini sharti ni atawadhe baada ya kuingia wakati wa swalah, kama ilivyo kwa mwanamke mwenye damu ya ugonjwa. Ikiwa chupi yake ina najisi, aioshe au aibadilishe. Lakini ikiwa najisi imetokea ndani ya swalah, hakuna tatizo muda wa kuwa bado yumo ndani ya wakati wa swalah mpaka wakati utoke.

Swali: Kwa hivyo, anatanguliza kufunika uchi kuliko kujiepusha na najisi?

Jibu: Ndiyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31577/ما-يفعل-من-به-سلس-فيما-يصيب-ثوبه-اثناء-الصلاة
  • Imechapishwa: 07/11/2025