Cha lazima ni mwili mzima upate maji

Swali: Je, ni lazima kusugua mwili mzima kwa mikono wakati wa kuoga josho la janaba au inatosha kuumwagilia maji tu?

Jibu: Inatosha kuumwagilia maji na kuyaeneza juu ya mwili mzima wakati wa kuoga janaba, hedhi na damu ya uzazi. Hayo ni kutokana na kuenea kwa Hadiyth na Aayah juu ya hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/187)
  • Imechapishwa: 29/08/2021