Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

“Utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi.”[1]

Sulaymaan bin Swurad amesema:

”Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati ambapo wanaume wawili wakitukanana. Mmoja wao uso wake umekuwa mwekundu na mishipa ya shingo yake ikavimba. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Hakika ninajua neno ambalo akilisema yataondoka hayo anayoyapata. Akisema:

أعوذ بالله من الشيطان الرجيم

”Najikinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa.”

yatamwondokea.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

´Aṭwiyyah bin ´Urwah amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ghadhabu inatokana na shaytwaan na shaytwaan ameumbwa kutokana na moto. Hakika mambo yalivyo ni kwamba moto huzimwa kwa maji. Basi mmoja wenu anaposhikwa na ghadhabu basi na atawadhe.”[3]

Ameipokea Abu Daawuud.

Abu Dharr ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mmoja wenu anapoghadhibika ilihali amesimama, basi na aketi chini. Ikiwa hasira itaondoka ni sawa. Vinginevyo alale chini.”[4]

[1] 41:36

[2] al-Bukhaariy (3282) na (6048) na Muslim (2610).

[3] Abu Daawuud (4784) na Ahmad (6/168). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “adh-Dhwa´iyfah” (582).

[4] Abu Daawuud (4782). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4782).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 362
  • Imechapishwa: 10/09/2025