689 – Nilimuuliza Shaykh wetu bwana wa du´aa[1] maana yake ni kwamba du´aa hiyo ndio kubwa zaidi ya msamaha?

Jibu: Ndio.

[1] Buraydah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Bwana wa du´aa ya msamaha ni:

اللهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لا إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبوءُ لَكَ بِنِعْمَتِك عَلَيَّ وأَبوءُ بِذَنْبِي فاغْفِرْ لي فإِنَّه لاَ يغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ

“Ee Allaah! Wewe ni Mola wangu. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe. Umeniumba mimi na mimi ni mja wako. Nami niko juu ya ahadi Yako na agano lako kiasi cha uwezo wangu. Najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya. Nakiri Kwako kwa kunineemesha. Nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehi madhambi isipokuwa Wewe.” (al-Bukhaariy (6323)).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 246
  • Imechapishwa: 03/07/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´