Bora zaidi kuoa mwanamke wa Kiislamu kuliko kuoa Ahl-ul-Kitaab

Swali: Je, inajuzu kwa muislamu kuoa wanawake wa kiyahudi na wa kinaswara katika mji wa Kiislamu?

Jibu: Jambo la kwanza, mimi siwezi kuharamisha jambo ambalo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Kalifanya kuwa halali. Allaah (´Azza wa Jall) karuhusu kuoa wanawake wa Ahl-ul-Kitaab, sawa akiwa ni myahudi au mnaswara. Kwa sharti mwanamke huyo awe ni katika al-Muhswanaat, yaani wanawake watwaharifu wenye kujisitiri na sio makahaba.

Jambo la pili, mimi kama ningelikuwa mwenye kuhukumu ningeliwakatalia wanaume kuwaoa wanawake wa Ahl-ul-Kitaab. Kwa nini? Sisemi kwa njia ya kuharamisha, lakini kwa kukithiri wanawake wa Kiislamu ambao hawajaolewa manyumbani. Kukimbilia kuoa wanawake wa Ahl-ul-Kitaab, linazuia kuoa wanawake Waislamu. Dada yako ambaye ni Muislamu ni aula zaidi kwako na wewe ni aula zaidi kwake.

Kisha jambo lingine, unatakiwa kumfanya huyo mwanamke wa kitabu aweze kusilimu, unatakiwa vilevile umpate mwanamke wa kitabu asiyefitini. Bali kuko wanawake ambao wanakwenda mpaka na watoto wao mpaka kwa watu wao. Na mimi naelezea jambo nilijualo na visa vinanifikia kutoka kwa watu waaminifu. Ninawaita enyi wanaume wa Kiislamu msioe wanawake wa Ahl-ul-Kitaab. Nimetangulia kusema ya kwamba mimi siharamishi hili. Lakini ni kwa ajili ya maslahi.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/4014
  • Imechapishwa: 22/09/2020