Bora kwenda kuhiji tena au kumsafirisha ambaye hajahiji?

Swali: Mimi ni kijana ambaye nimeshahiji zaidi ya mara moja. Ni lipi bora hivi sasa; nihiji mwenyewe tena au nimpe  gharama za pesa muislamu ambaye bado hajahiji hajj ile hajj ya kwanza ambayo ni faradhi?

Jibu: Bora ni wewe kumpa ambazo atatekeleza hajj ya faradhi. Huenda ukaandikiwa  thawabu mfano wake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuandaa jeshi naye amepigana na mwenye kumbakilia kwa ajili ya familia yake kwa wema amepigana.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (62) http://binothaimeen.net/content/1395