Bora kwenda katika swalah ya ijumaa kwa kutembea au kwa gari?

Swali: Ni lipi bora kuhusu kwenda katika swalah ya ijumaa; mtu aende kwa kutembea au aende na gari?

Jibu: Bora ni kwenda msikitini kwa kutembea kama ilivyokuja katika Hadiyth juu ya fadhila zinazopatikana katika kwenda ijumaa:

“Atakayeenda kwa muda na mapema… “

Katika baadhi ya mapokezi yake:

“… akatembea na asipande, akawa karibu na imamu, asifanye upuuzi na akasikiliza, anasamehewa yaliyo kati yake na ijumaa nyingine na kuongezea siku tatu.”

Ikiwa ni wepesi kwake kutembelea ndio bora zaidi. Ikiwa msikiti uko mbali na akapanda gari kunatarajiwa kwake kheri. Lakini kule kutembea ikimsahilikia ndio bora zaidi ikiwa hilo si gumu kwake. Ikiwa ni jambo gumu kwake au msikiti ukawa mbali basi yuko katika kheri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 29/12/2017