Bora kwa mgonjwa asiwaombe watu kumtabana

Swali: Je, bora kwa mgonjwa ni kuacha kuomba kufanyiwa matabano?

Jibu: Ndio bora. Isipokuwa haja ikimpelekea kufanya hivo. Ni kama ambavo zinamuwepesikia sababu nyenginezo. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha kufanya matabano kutokana na kijicho. Ni kama kujitibu kwa kujichoma kwa chuma cha moto. Bora ni kuacha kufanya hivo, kwa sababu inachukiza. Hata hivyo mtu akihitajia kufanya hivo yale machukizo yanaondoka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24376/هل-الافضل-للمريض-ترك-طلب-الرقية
  • Imechapishwa: 03/10/2024