Bora kuzisoma mwanzoni mwa usiku

Swali: Vipi kuhusu kusoma Aayah mbili za mwisho za Suurah ”al-Baqarah”?

Jibu: Katika mwanzo wa usiku. Mwenye kuzisoma mwanzoni mwa usiku, basi zinamtosheleza. Inahusiana na Aayah mbili za mwisho za Suurah ”al-Baqarah”. Mwenye kuzisoma katika usiku, basi zinamtosheleza. Azisome mwanzoni mwa usiku au katika katikati ya usiku. Imepokelewa kuwa ni mwanzoni mwa usiku. Bora zaidi ni kuzisoma mwanzoni mwa usiku.

Swali: Kabla ya kulala?

Jibu: Katika mwanzo wa usiku, kwa maana kabla ya kulala. Bora azisome mwanzoni mwa usiku. Afanye haraka kuzisoma mwanzoni mwa usiku.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27635/متى-يستحب-قراءة-الايتين-اخر-سورة-البقرة
  • Imechapishwa: 06/04/2025