Swali: Mtu ajifanyie mwenyewe matabano au amwombe mwengine amtabanie?
Jibu: Akijifanyia mwenyewe matatano ni sawa, na ikiwa atamwomba mtu mwingine ni sawa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimwamrisha ´Aaishah afanye matabano. Aidha alimwamrisha mama wa watoto wa Ja’far kuwafanyia matabano watoto wa Ja’far. Kwa hivyo hapana vibaya. Ikiwa atajifanyia mwenyewe matabano, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akijifanyia mwenyewe matabano.