Swali: Ni ipi ufumbuzi kuhusu jirani muovu anaposhauriwa lakini isifue dafu. Je, ahame kutoka maeneo hayo akiweza au amvumilie?

Jibu: Afanye kile chenye manufaa zaidi. Ikiwa kuishi kwake maeneo fulani ndio kheri zaidi basi avumilie huku akimnasihi, awakumbushe watu na awalinganie watu kwa Allaah. Na ikiwa kuhamia kwake mahali pengine ndio kuna manufaa zaidi basi ahame.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24344/هل-الافضل-الانتقال-عن-جار-السوء-ام-الصبر
  • Imechapishwa: 01/10/2024