Bora kufanya Adhkaar kwa kwa sauti ya juu au kimyakimya?

Swali: Je, ni bora kutaja Dhikr kwa sauti ya juu au kimyakimya?

Jibu: Amtaje Allaah kwa utajo unaosikiwa na walioko karibu yake ili anufaike yeye mwenyewe na wanufaike watu wengine, isipokuwa katika swalah. Akimaliza swalah na kutoa salamu ainue sauti yake; kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiinua sauti yake baada ya kumalizika swalah. Vilevile Maswahabah walikuwa wakinyanyua sauti zao baada ya kumaliza swalah. Ama katika nyakati nyingine za kawaida, aseme kwa sauti kiasi cha kujisikia yeye na wale waliokaribu naye ili waweze kumfuata, kama vile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akimtaja Allaah na Maswahabah wakimsikia na kumuigiliza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31170/هل-الافضل-الجهر-بالاذكار-ام-الاسرار
  • Imechapishwa: 09/10/2025