Swali 31: Ni ipi hukumu kwa mkazi wa Makkah kufanya ´Umrah? Je, ni Bid´ah kama ilivyosemwa?
Jibu: Manneo haya yaliyosemwa na muulizaji wameonelea hivo baadhi ya wanazuoni na wakasema kwamba mkazi wa Makkah hana ´Umrah. Lakini dhahiri ya dalili iko kinyume na hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema alipoweka vituo:
”Hizo ni kwa ajili yao na kwa ajili ya yule anayepita kupitia huko kutoka wasio wakazi wake kwa yule anayekusudia Hajj au ´Umrah. Yule aliyeko karibu zaidi na hilo, basi kutoka pale alipoanzia, mpaka watu wa Makkah kutoka Makkah.”[1]
Hii inafahamisha kwamba ´Umrah inaweza kuwa kwa watu wa Makkah. Lakini ikiwa wanataka kufanya ´Umrah, basi ni lazima watoke kwenda Tan´iym au sehemu nyingine ya nje ya Makkah ili waingie ndani ya Ihraam kutoka huko. Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
[1] al-Bukhaariy (1526) na Muslim (1181).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/36-37)
- Imechapishwa: 08/05/2026
Swali 31: Ni ipi hukumu kwa mkazi wa Makkah kufanya ´Umrah? Je, ni Bid´ah kama ilivyosemwa?
Jibu: Manneo haya yaliyosemwa na muulizaji wameonelea hivo baadhi ya wanazuoni na wakasema kwamba mkazi wa Makkah hana ´Umrah. Lakini dhahiri ya dalili iko kinyume na hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema alipoweka vituo:
”Hizo ni kwa ajili yao na kwa ajili ya yule anayepita kupitia huko kutoka wasio wakazi wake kwa yule anayekusudia Hajj au ´Umrah. Yule aliyeko karibu zaidi na hilo, basi kutoka pale alipoanzia, mpaka watu wa Makkah kutoka Makkah.”[1]
Hii inafahamisha kwamba ´Umrah inaweza kuwa kwa watu wa Makkah. Lakini ikiwa wanataka kufanya ´Umrah, basi ni lazima watoke kwenda Tan´iym au sehemu nyingine ya nje ya Makkah ili waingie ndani ya Ihraam kutoka huko. Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
[1] al-Bukhaariy (1526) na Muslim (1181).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/36-37)
Imechapishwa: 08/05/2026
https://firqatunnajia.com/bidah-kwa-mkazi-wa-makkah-kufanya-umrah/