Bid´ah inayofanywa na wengi baada ya swalah

Swali: Vipi kwa mfano wakati wa kuomba du´aa baada ya swalah ya faradhi akaomba du´aa kwa kunyanyua mikono juu kisha akapangusa uso wake?

Jibu: Hapana, hilo ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Baada ya faradhi hakunyanyuliwi mikono juu. Hata hivyo ni sawa akiomba baina du´aa baada ya faradhi baina yake yeye na nafsi yake.

Swali: Anyanyua mikono yake na anasema kuwa ni Bid´ah?

Jibu: Haya ni maovu. Hiyo ni Bid´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1071/رفع-اليدين-بالدعاء-بعد-الفريضة
  • Imechapishwa: 24/01/2026