Biashara ya mwanamke ambapo anahitajia kuzungumza na wanaume

Swali: Mume anayemkataza mke wake biashara inayohitajia kuwazungumzisha wanamme ambao sio Mahram zake. Je, mume ni mwenye kukosea kwa kumkataza?

Jibu: Biashara ya mwanamke na kutoka kwake kwenda sokoni hakukui isipokuwa kwa kupatikana mambo mawili:

1- Afanye kazi za nyumbani na kazi za nyumbani zisikose wa kuzifanya. Kazi za nyumbani ni jukumu lake. Kazi za nyumbani zisikose wa kuzifanya na akatoka na kuziacha.

2- Ni lazima amtii mume. Bi maana asitoke isipokuwa kwa idhini yake. Asitoke nyumbani kwake isipokuwa kwa idhini yake.

Yakipatikana masharti haya mawili inajuzu kwake kutoka na kufanya biashara.

Kuhusiana na mwanamke kumzungumzisha mwanaume kwa haja kwa maneno ya kawaida, kumuuliza kuhusu elimu, masuala fulani n.k., hakuna ufedhuli, kulegeza sauti na fitina, haina neno. Inatakiwa iwe kwa haja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (58) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020