Swali: Imeenea aina ya uwekezaji uutwao “kikapu cha sarafu” ambapo mtu anaipa benki pesa pamoja na uwakala ili benki ifanye biashara ya kununua na kuuza sarafu kwa niaba yake. Ni ipi hukumu ya hili?
Jibu: Kama ilivyotajwa, mtu anaipa benki au mtu mwingine pesa ili afanye biashara ya sarafu kwa niaba yake. Biashara ya sarafu ina ufafanuzi:
Ikiwa inafanyika kwa njia ya ribaa, basi ni haramu. Ikiwa inafanyika kwa njia ya Shari´ah, basi inajuzu. Hivyo ikiwa sarafu inauzwa kwa sarafu nyingine kwa mkono kwa mkono, hakuna ubaya. Ni kama kuuza dola kwa pauni ya Uingereza, pauni ya Misri au SAR ya Saudia, kwa kukabidhiana hapo hapo, hilo linajuzu. Ama ikiwa ni kwa kucheleweshwa au bila kupokeleana katika kikao kimoja, basi hilo halijuzu. Kwa sababu sarafu zinachukuliwa kama fedha na zina hukumu yake katika maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Dhahabu kwa dhahabu ni ribaa isipokuwa mkono kwa mkono.”
Imekuja katika tamko jengine:
“Dhahabu kwa fedha ni ribaa isipokuwa mkono kwa mkono.”
“Fedha kwa fedha ni ribaa isipokuwa mkono kwa mkono.”
“Ngano kwa ngano ni ribaa isipokuwa mkono kwa mkono.”
“Shayiri kwa shayiri ni ribaa isipokuwa mkono kwa mkono.”
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Dhahabu kwa dhahabu sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, na fedha kwa fedha sawa kwa sawa, mkono kwa mkono.”
Vilevile ametaja ngano, shayiri, tende na chumvi, vyote kwa mkono kwa mkono na sawa kwa sawa.
Kwa hiyo sarafu zinazotumika na watu, ikiwa zinabadilishwa kwa kukabidhiana papo hapo na ni za aina tofauti, basi hakuna ubaya kama dola kwa pauni, dola kwa dinari ya Jordan au dinari ya ´Iraaq muda wa kuwa ni mkono kwa mkono. Ama dola 1 kwa dola 2, haijuzu. Hiyo ni ribaa ya ziada. Ikiwa ni kwa kucheleweshwa, basi zinakusanyika aina mbili za ribaa: ribaa ya ziada na ribaa ya kucheleweshwa. Kadhalika ikiwa atauza sarafu ya Saudia 10 kwa 11, 10 kwa 12 hata kama ni papo hapo, hiyo ni ribaa ya ziada. Ikiwa ni kwa kucheleweshwa, basi zinakusanyika aina zote mbili za ribaa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3216/حكم-الاتجار-بالعملات
- Imechapishwa: 20/10/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3216/حكم-الاتجار-بالعملات
Imechapishwa: 20/10/2026
https://firqatunnajia.com/biashara-ya-kuchenchi-pesa/