Hapana vibaya kuwakumbatia Mahram zako

Swali: Je, inajuzu kukumbatiana na kukutana na mama mdogo, shangazi na mfano wa watu hawa?

Jibu: Ndiyo, hao ni Mahram. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipomjia msichana wake Faatwimah, basi anasimama kwa ajili yake, anamshika mkono wake na kumbusu. Hivyo akimjia shangazi yake, mama yake, mama yake mdogo au dada yake, akisimama kwa ajili yake na kumsalimia kwa mkono au kumkumbatia, hakuna ubaya katika hilo.

Swali: Vipi kuhusu mke wa ami yake?

Jibu: Hapana, mke wa ami yake si Mahram.

Swali: Je, anaweza kukutana naye?

Jibu: Mke wa ami yake, mke wa ndugu yake na mke wa mjomba wake si Mahram kwake. Anachofanya ni kumsalimia kwa maneno tu bila kushikana mkono wala kukumbatiana, kwa kusema ”Vipi hali yako? Watoto wanaendeleaje? Ami yangu anaendeleaje? Mjomba wangu anaendeleaje?” Ama kumbusu au kushikana mkono, hapana.

Swali: Je, kukutana naye kunajuzu?

Jibu: Kukutana kuna aina: kukutana kwa mazungumzo hakuna ubaya ikiwa amejisitiri kwa Hijaab. Ama kukutana kwa kushikana mkono, kukumbatiana au kumbusu, hapana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3212/حكم-معانقة-المحارم
  • Imechapishwa: 20/10/2026