Swali: Je, biashara siku nyingine zisizo ya ijumaa inajuzu baina ya adhaana na Iqaamah?

Jibu: Ni vyema kuiacha, kwa sababu inaweza kumzuia mtu na swalah. Ingawa dalili maalum ni kwa ajili ya ijumaa, lakini katika siku nyingine pia ni vyema mtu aache ili asizuiliwe na swalah. Kilicho bora na cha tahadhari zaidi kwake ni kuiacha. Hata kama andiko lipo kwa ajili ya ijumaa, lakini tahadhari zaidi kwa muumini ni kuiacha biashara pale anaposikia mwito wa swalah; ni mamoja iwe ni Dhuhr, ´Aswr, Maghrib au ´Ishaa. Kwa kuwa swalah zote zinafanana katika maana; zote ni faradhi na zote ni wajibu kuziharakia. Hivyo ingawa maandiko yanahusu ijumaa na yanaonyesha ukubwa wa hadhi ya ijumaa, lakini haimaanishi kwamba nyingine hazina uzito. Kwa hivyo muumini ajitahidi pindi anaposikia adhaana, basi aharakie. Hilo ndilo salama zaidi kwa muumini.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31560/حكم-البيع-بين-الاذان-والاقامة-في-غير-الجمعة
  • Imechapishwa: 02/11/2025