Baruka ni mbaya zaidi kuliko kuunganisha nywele kwa nyuzi

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa baruka kwa mwanamke au mwanaume mwenye kasoro ya upara ni ipi? Ni ipi hukumu ya kuziuza kwenye maduka?

Jibu: Kuvaa wigi ni jambo baya zaidi kuliko kuunganisha nywele. Kuunganisha nywele ni kuongeza nywele juu ya nywele. Tusemeje kuhusu kuvaa wigi ambayo ni kama kichwa kizima? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwahi kushika fundo la nywele na kusema:

”Hakika si vyenginevyo waliangamia wanawake wa wana wa israaiyl kwa sababu walifanya mambo kama haya.”

Kwa hiyo kudanganya kwa namna hiyo hakufai. Lakini tiba ya kurudisha nywele kwa matibabu halali haina tatizo. Kwa maana ya kwamba kujitibu ili nywele zikue upya, hilo halina shida. Ama kuvaa fundo la nywele bandia au kuunganisha nywele, hilo halijuzu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30973/حكم-الباروكة-لمن-به-صلع-من-النساء-والرجال
  • Imechapishwa: 24/09/2025