Swali: Ni ipi hukumu ya kula nyama zinazoletwa kutoka nje kwa sababu baadhi ya watu wanasema kuwa hawachinji kwa njia ya Kishari´ah?

Jibu: Ziepuke. Nyama zinazochinjwa hapa kwetu ni zenye kutosheleza na himdi zote ni za Allaah. Na kama uko katika nchi ya nje achana nazo na badala yake kula samaki. Sio lazima ule nyama. Kula chakula na mboga mboga kwa ajili ya usalama katika dini yako. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Achana na kile chenye kukutia shaka na ukiendee kisichokutia shaka.”

Nchi za nje kuna waislamu wachache wenye kuchinja kwa njia ya Kishari´ah. Waulizie. Wana maduka yao. Nenda na ununue kwao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-09.mp3
  • Imechapishwa: 25/05/2018