Baba anauomba mwanae amsomee matabano

Swali: Baba akimuomba mtoto wake amsomee Ruqyah ni jambo linaloingia katika Hadiyth[1] au mtoto wake ni katika chumo lake?

Jibu: Inaingia katika Hadiyth. Kuacha kumuomba ni bora zaidi. Jisomee mwenyewe.

[1] Huswayn bin ´Abdir-Rahmaan amesimulia:

“Nilikuwa kwa Sa´iyd bin Jubayr na akasema: “Ni nani kati yenu aliyeona nyota iliyorushwa jana?” Nikasema: “Mimi niliiona”, kisha nikasema kwamba haikuwa katika Swalah kwa kuwa nilidonolewa na nge.” Akasema: “Ulifanya nini?” Nikasema: “Nilitumia Ruqyah ili kujiponyesha.” Akasema: “Kipi kilichokupelekea ufanye hivyo?” Nikasema: “Ni kutokana na Hadiyth aliyotuelezea Sha´biy.” Nikasema: “Kawaeleza nini?” Nikasema: “Katueleza kutoka kwa Buraydah bin Huswayb ya kwamba kasema: “Hakuna Ruqyah isipokuwa kwa kupatwa na kijicho au kudonolewa.” Nikasema [Sa´iyd bin al-Jubayr]: “Amefanya vizuri kusitisha alichokisikia. Lakini katuhadithia Ibn ´Abbaas, ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kuwa kasema: “Ummah zote zilipitishwa mbele yangu, nikamuona Mtume Mtume akiwa hana mtu yeyote. Kisha nikaonyeshwa idadi kubwa ya watu niliodhania ni katika Ummah wangu, lakini nikaambiwa: “Huyo ni Muusa na watu wake.” Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa, ambalo nikaambiwa: “Hawa ni watu wako, miongoni mwao ni watu elfu sabiini watakaoingia Peponi bila ya kufanyiwa hesabu wala adhabu.” Kisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akaondoka kwenda nyumbani kwake na nyuma yake watu wakaanza kujadiliana ni nani hao watakaoweza kuwa? Baadhi yao wakasema: “Pengine ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).” Na baadhi yao wengine wakasema: “Pengine ni wale waliozaliwa katika Uislamu na hawakumshirikisha Allaah kwa chochote.” Walipokuwa wakijadiliana, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akatoka na kuja na wakamwambia [waliyokuwa wakiyajadili]. Akasema: “Ni wale ambao wasiojitibu kwa Ruqyah, wala kujichoma chuma cha moto, wala hawaamini rajua nzuri na mbaya, bali wanamtegemea Mola Wao Pekee.” ‘Ukkaashah bin Mihswan (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliposikia alisimama akasema: “Muombe Allaah Anijaalie kuwa mmoja wao.” Akasema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Wewe ni katika wao.” Kisha akasimama mtu mwengine na akasema: “Muombe Allaah Anijaalie kuwa mmoja wao”. Akasema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Amekutangulia ´Ukkaashah.” (Kitaab-ut-Tawhiyd cha Imaam Ibn ´Abdil-Wahhaab)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (15) http://alfawzan.af.org.sa/node/2108
  • Imechapishwa: 05/07/2020