Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anaamrishwa na baba yake kumnunulia sigara, tumbaku au mirungi?

Jibu: Asimtii. Hakika mambo yalivyo ni kwamba utiifu unakuwa katika yaliyo mema. Bali unapaswa kumnasihi baba yako na kumfayia upole. Kuna tofauti kati ya mwanafunzi na mtu wa kawaida. Hata kama ni mkubwa kukushinda, wewe ni mwanafunzi na hivyo nataraji ukawa na akili na busara kumshinda. Uelewa na maadili yake mema yanakuwa. Mtendee wema na mweleze kuwa hukubalieni naye na kwamba unamnasihi kuachana na jambo hilo.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 217
  • Imechapishwa: 15/02/2025